KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

TMK Wanaume Halisi yatema wasanii saba



KUNDI la muziki wa kizazi kipya la TMK Wanaume Halisi limeamua kuwatema wasanii wake saba na kubaki na watano.

Kiongozi wa kundi hilo, Juma Kassim ‘Nature’ alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, uamuzi wao huo umetokana na matakwa ya wadhamini wao wapya.

Nature alisema kundi hilo hivi karibuni limeingia mkatabawa udhamini na Kampuni ya DLC, ambayo inafanya biashara zake katika nchi za Tanzania na China.

Alisema kampuni hiyo itakuwa ikisimamia kazi zote za kundi hilo, ikiwa ni pamoja na kulitangaza ndani na nje ya nchi na kuliandalia maonyesho na matamasha ya muziki.

“Tulipata wakati mgumu sana katika kuchuja vichwa 12 vilivyomo ndani ya kundi ili kubaki na vitano, ambavyo ndivyo vitakavyofanyakazi na kampuni hiyo,”alisema Nature.

Mbali na yeye, alivitaja vichwa vingine vinne vilivyobaki kwenye kundi hilo kuwa ni Dolo, Baba Levo, JB wa Mabaga Fresh na KG Son.

Kundi la TMK Wanaume Halisi lilianzishwa mwaka jana baada ya baadhi ya wasanii wakiongozwa na Nature kujiengua katika kundi la TMK Wanaume Family.

Kundi hilo lilijipatia sifa na umaarufu baada ya kuibuka na albamu yake ya kwanza, inayoitwa ‘Tatu bila’. Hivi sasa kundi hilo lilikuwa likijiandaa kuipua albamu yake ya pili, itakayojulikana kwa jina la ‘Mnatakaje?’

No comments:

Post a Comment