KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

Genevieve ajitosa kimapenzi kwa D'Banj








LAGOS, Nigeria
KATIKA kile kinachoonekana kuwa ni taarifa ‘babu kubwa’ kuliko zote zilizoripotiwa mwaka huu nchini Nigeria, imebainika kuwa, mwigizaji nyota wa filamu wa Nollywood, Genevieve Nnaji na mwanamuziki maarufu wa nchi hiyo, D’Banj wana uhusiano wa kimapenzi.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimebainisha wiki hii kuwa, wapenzi hao wawili wamekuwa wakikutana mara kwa mara kwa siri kabla ya kufumwa na macho ya ‘mapaparazi’ wa nchi hiyo.
Kwa kuona kwamba hiyo ingekuwa dili kwao ya kutengeneza fedha, ‘mapaparazi’ hao waliwategea mtego wapenzi hao wawili wa kuwatoa ‘noti’ ili taarifa hizo zisiripotiwe kwenye vyombo vya habari,lakini walishtuka.
Ndipo D’Banj alipoamua kuzitoa taarifa hizo yeye mwenyewe kwenye vyombo vya habari, kupitia kwa mwandishi Stella Dimoko-Korkus wa Nigeria.
Akihojiwa na mwandishi huyo, D’Banj alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na Genevieve na kusisitiza kwamba, hiyo ilikuwa siri kubwa kwao.
“Sielewi nitumie maneno gani mengine kuelezea hisia zangu, lakini utakapoiona video ya wimbowangu niliyorekodi naye, utaelewa kwamba si video tu, ilikuwa ni mimi nikizungumza na mpenziwangu kiukweli,”alisema D’Banj.
Mwanamuziki huyo alikanusha madai kuwa, amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanawake wengi, baadhi yao wakiwa watu maarufu. Pia alikanusha kufanya mapenzi kabla ya kupanda stejini na baada ya onyesho.
“Hayo yote hayana ukweli wowote, ni kama ulivyosema kwamba ni uvumi tu. Lakini mpenzi wangu halisi ni Genevieve na hii ni mara ya kwanza kumtangaza kwa sababu ni habari za ukweli,”alisema.
Hata hivyo, D’Banj hakuwa tayari kueleza iwapo anatarajia kufunga ndoa na mwigizaji huyo nyota wa Nollywood na kusisitiza kuwa, kwa sasa bado ni mpenzi wake.
“Sote wawili ni watu tuliopevuka na tunapenda kufanya mambo yetu kwa siri. Kuna tofauti kubwa kati ya maisha yetu ya hadharani na ya faragha. Tungependa uhusiano wetu uende hatua kwa hatua hadi muda utakapowadia na tutafurahi kama watu wataacha kutufuatilia kwa wakati huu,”alisema mwanamuziki huyo.
Je, D’Banj yupo tayari kuona taarifa za uhusiano wao zikitapakaa mitaani na habari za mahusiano yake na wanawake wengine zikichapishwa mara kwa mara kwenye magazeti? Yeye na Genevieve wamejiandaaje kwa hilo?
"Niseme nini? Kama nilivyosema, Genevieve ni msanii nyota wa Afrika ninayemfahamu na mimi pia najulikana na watu wengi, hivyo hilo ni jambo linalotarajiwa kutokea, lakini sijali kuhusu taarifa yoyote itakayotoka hadharani, kama nilivyokueleza, nilishavumishiwa kuwa na uhusiano na watu kadhaa, ambao sijawahi kukutana nao,”alisema.
D’Banj alisema anaona fahari kuwa na uhusiano na mwigizaji huyo mwenye sura yenye mvuto na
kuongeza kuwa, siku alipokutana naye, alielewa kile anachokihitaji na hadi sasa yupo nacho.
“Ni mwanamke ninayemuhitaji. Wanaweza kusema chochote wanachopenda. Watu wananielewa mimi kama mburudishaji na nitafanya kile ninachokifanya ninapokuwa stejini na nje ya steji, naishi maisha yangu binafsi,”alisema.
“Watu wanadhani wananifahamu vyema, wanasema vitu vingi, lakini hakuna anayeelewa vyemachochote kuhusu mimi na ninapenda kuishi hivyo,” aliongeza.
“Kwa sasa, mwanamke pekee aliyoko maishani mwangu ni Genevieve na anafahamu hivyo. Hatuelewi kuhusu kesho, lakini tunataka kuwa pamoja na hatutaki kuendelea kuficha ukweli kuhusu hilo. Nataka kutoka naye matembezini, kwenda naye mahali popote na si kuficha. Sote hatuna wenza, hivyo hatufanyi kosa lolote,” aliongeza.

No comments:

Post a Comment