KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

Diamond alia traki yake kuvuja


MSANII nyota chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Diamond amevilalamikia baadhi ya vituo vya radio nchini kwa kupiga kibao chake kipya bila ridhaa yake.

Diamond alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, alikuwa akijiandaa kuachia ‘traki’ yake hiyo hivi karibuni, lakini alishangaa kuisikia ikipigwa redioni kabla ya kuikabidhi kwenye vituo hivyo.

“Hiyo nyimbo bado sijaitoa kwenye kituo chochote cha radio, lakini nashangaa imeshaanza
kupigwa,”alilalamika msanii huyo.

Kwa mujibu wa Diamond, kibao chake hicho kinajulikana kwa jina la ‘Mbagala’.Alisema kutokana na traki hiyo kuvuja mapema, ameamua kuipiga upya, ikiwa ni pamoja na kujiandaa
kurekodi video yake.

“Kwa taarifa yao ni kwamba, video na audio ya wimbo huu sasa itakuwa tofauti na ile
iliyovuja,”alisema.

Katika hatua nyingine, msanii AT anatarajia kuipua albamu yake mpya hivi karibuni. Albamu hiyo itajulikana kwa jina la ‘Nipigie’.

AT alisema wiki hii kuwa, albamu yake hiyo itawashirikisha wakali kibao wa muziki huo, ambao
hakuwa tayari kutaja majina yao.

No comments:

Post a Comment