MWIGIZAJI nyota wa filamu nchini, Blandina Chagula ‘Johari’ amepinga madai kuwa, filamu nyingi zinazotengenezwa nchini, maudhui yake ni ya kuiga kutoka katika filamu za Kinigeria.
Akizungumza mjini Dar es Salaam wiki hii, Johari alisema kauli za aina hiyo zinawakatisha tamaa
wasanii wa filamu, badala ya kuwapa ari ya kuwa wabunifu zaidi.
Johari alisema wadau wengi wa filamu nchini wamekuwa wakitazama mambo mabaya kwa kilakinachofanywa na wasanii wa Tanzania na kuyafumbia macho mambo mazuri.
Alisema watu wanaowaponda wasanii wa filamu wa Bongo hawaelewi wanachozungumza nahawatazami juhudi zinazofanywa na wasanii hao katika kuiendeleza fani hiyo.
Msanii huyo amewataka wadau wa filamu nchini kuacha kutoa kauli za kuwaponda, badala yakewawasifu kila wanapofanya mambo mazuri.
“Hatukatai kukosolewa, lakini iwe kwa nia njema ya kujenga na si kuponda kila kitu kinachofanywa na msanii wa filamu wa Tanzania,”alisema.
Katika hatua nyingine, mwigizaji nyota wa vichekesho nchini, King Majuto amewaponda watayarishaji wa filamu kwa kuigiza mapenzi zaidi na kuacha matukio mengine muhimu katika jamii.
Majuto alisema mjini Dar es Salaam kuwa, hupatwa na hasira kila anapowaona waigizaji wa Tanzania wakiigiza mapenzi kwenye filamu zao wakati yapo matukio mengi ya kusisimua.
"Kila ukitazama filamu, utakutana na masuala ya mapenzi tu, kwani hakuna mambo mengine? Umefika wakati suala hilo linakinai kulitazama,”alisema."Ni kweli mapenzi yana nafasi yake katika jamii, lakini ni vema yasipewe nafasi kubwa, tunapaswa kwenda na wakati,”alisema mwigizaji huyo, aliyeanza kujihusisha na fani hiyo tangu miaka ya 1970.

No comments:
Post a Comment