KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, April 20, 2010

Simba ilipoiadhiri Yanga

HIVI tutashinda kweli leo! Ni Meneja wa Simba, Innocent Njovu (kushoto) na Kocha Msaidizi, Amri Saidi walipokuwa wakijadiliana jambo kabla ya mechi kati yao na Yanga
TWENDE ukakabidhi kombe. Ndivyo inavyoelekea Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga (kushoto) akimueleza Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya.

MASHABIKI wa Simba wakifuatilia kwa makini pambano kati yao na Yanga. Simba ilishinda mabao 4-3.
WACHEZAJI Shadrack Nsajigwa (kushoto) wa Yanga na Juma Jabu (kulia) wa Simba wakigombea mpira timu hizo zilipomenyana katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

MSHAMBULIAJI Mussa Hassan 'Mgosi' (kulia) akitafuta mbinu za kumtoka kiungo Athumani Idd 'Chuji' wa Yanga timu hizo zilipomenyana katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WACHEZAJI wa Simba wakifurahia kombe walilokabidhiwa baada ya timu hiyo kuibamiza Yanga mabao 4-3 katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

WACHEZAJI wa Simba wakipongezana baada ya timu yao kuicharaza Yanga mabao 4-3 katika mechi ya ligi kuu ya soka ya Vodacom iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
WACHEZAJI wa Simba wakiwa wamembeba kocha wao msaidizi, Amri Saidi baada ya timu hiyo kuichapa Yanga mabao 4-3 katika mechi ya ligi kuu ya Vodacom iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment