KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

PAPIC-Siwezi kuitosa Yanga



KOCHA Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic amesema hana mpango wa kuitosa timu hiyo hadi mkataba wake utakapomalizika.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Dar es Salaam jana, Papic alisema mkataba wake wakuifundisha Yanga unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom.
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kumalizika Machi 27 mwaka huu, ambapo Yanga imesaliwa na mechi nne dhidi ya Azam, Moro United, Simba na Prisons.Yanga inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo, ikiwa na pointi 24 baada ya kucheza mechi 18. Simba inaongoza kwa kuwa na pointi 50 kutokana na idadi hiyo ya michezo.
Msimamo huo wa Papic umekuja baada ya kuwepo na taarifa kwamba, ameamua kufungasha virago kutokana na uongozi wa Yanga kushindwa kutekeleza majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kumlipa mshahara kwa wakati.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Papic alipanga kuzungumza na waandishi wa habari leo kuelezeamustakabali wake ndani ya klabu hiyo, yenye makao yake makuu mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Hata hivyo, kocha huyo amesema maamuzi ya kuondoka kwake yatategemea mabadiliko ya maendeleo ndani ya timu hiyo, iliyotolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuchapwa jumla ya mabao 4-2 na FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Papic alisema endapo hakutakuwa na mafanikio baada ya msimu huu kumalizika, uwezekano wakuendelea kuifundisha timu hiyo utakuwa finyu kwa vile malengo yake yatakuwa hayajatimia.
Kocha huyo kutoka Serbia alisema ni aibu kwake kuendelea kuifundisha timu, ambayo hajaipatia
mafanikio yoyote na kusisitiza kuwa, hilo ni miongoni mwa mambo yatakayomfanya afikiriekufungasha virago.
Alisema kocha mzuri ni lazima awe na malengo mazuri na kikosi chake na kuongeza kuwa, kufanya vibaya kwa timu yake hakuwezi kumfurahisha.
Papic alisema wakati alipoingia mkataba wa kuifundisha timu hiyo, yalikuwepo mambo mengi yamsingi, ambayo alikubaliana na uongozi yatekelezwe, lakini mengi hayajafanyiwa kazi.
Kocha huyo alitia saini mkataba wa kuifundisha Yanga kwa mwaka mmoja. Alitia saini mkataba huo Oktoba mwaka jana, akichukua nafasi ya kocha wa zamani, Dusan Kondic.
Tayari kocha huyo ameshahusishwa na mipango ya kuinoa timu ya taifa, Taifa Stars mara baada ya mkataba wa kocha wa sasa wa timu hiyo, Marcio Maximo kumalizika Juni mwaka huu.
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako amesema hana taarifa ya kuwepo kwa mkutano kati ya Papic na waandishi wa habari leo.
Mwalusako alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, Papic bado ni kocha wa Yanga na kama kunamatatizo, yatatatuliwa ndani ya vikao vya uongozi.
“Kama ameitisha mkutano na waandishi wa habari kesho (leo), sisi hatuna taarifa, lakini kiutendaji alitakiwa kutueleza, isipokuwa kama ameamua kufanya hivyo, basi atakuwa na lake la
moyoni,”alisema.
Akizungumzia suala la kucheleweshwa kwa mshahara wa kocha huyo, Mwalusako alisema uongozi hauna taarifa kwa vile analipwa na mfadhili mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji.
Kabla ya kutua Yanga, Papic aliwahi kuzinoa timu maarufu za Afrika zikiwemo Kaizer Chiefs, Maritzburg United na Orlando Pirates (Afrika Kusini), Lobi Stars, Enugu Rangers, Kwara United (Nigeria) na Hearts Of Oak ya Ghana.

No comments:

Post a Comment