KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 1, 2015

TOTO AFRICAN YAPIGWA 5-0 NA AZAM, KOCHA ABWAGA MANYANGA

Kocha Mkuu wa Toto African, Martin Grelics akiagana na wachezaji wake baada ya mchezo na Azam FC kwenye Uwanja wa Chamazi. Kocha amevunja mkataba na timu hiyo.
Wachezaji wa Toto African  wakiwa wamebeba ujumbe uliokuwa unasomeka 'Asante Sana Kocha Martin'
Beki wa Toto African, Salum Chuku (katikati) akichuana na mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu (wa pili kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Azam ilishinda 5-0.

KOCHA Mkuu wa Toto African ya Mwanza, Martin Grelics kutoka Ujerumani, ameamua kubwaga manyanga kuifundisha timu hiyo.

Martin alifikia uamuzi wake huo jana, muda mfupi baada ya Toto African kuchapwa mabao 5-0 na Azam katika mechi ya ligi kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi, Dar esSalaam.

Hakuna taarifa zaidi iliyotolewa kuhusu sababu za kocha huyo kubwaga manyanga,lakini wachambuzi wa masuala ya soka wameeleza kuwa, haridhishwi na usimamizi na uendeshaji wa timu hiyo.

Hivi karibuni, kocha huyo alikiri hadharani kuwa mwenendo mbaya wa timu hiyo katika ligi unatokana na wachezaji kutolipwa mishahara na pia kupata huzuma nzuri.

Ushindi wa jana uliiwezesha Azam kurejea tena kwenye uongozi wa ligi, uliokuwa ukishikiliwa na Yanga, ambayo juzi iliichapa Kagera Sugar mabao 2-0 mjini Tabora. Azam iko mbele kwa tofauti ya pointi mbili.


Katika mchezo huo, ambao wachezaji wa Toto waliingia na bango la kumuanga rasmi kocha wao, Mjerumani Martin, Azam FC walimaliza kipindi cha kwanza wakiwa wanaongoza 3-0.

Beki wa kulia Shomary Kapombe alifunga mabao mawili dakika za 34 na 36, akimalizia kazi nzuri ya winga Farid Mussa, wakati la tatu lilifungwa na Kipre Herman Tchetche dakika ya 45 akimalizia pasi ya kisigino ya Didier Kavumbangu.

Na mabao hayo yalikuja baada ya Toto kumpoteza kipa wake wa kwanza, Mussa Mohammed aliyeumia dakika ya 18 na nafasi yake kuchukuliwa na kipa wa pili, Said Omar.

Azam FC nayo ilipata pigo dakika ya 33 baada ya kiungo wake wa ulinzi, Himid Mao kuumia pia na nafasi yake kuchukuliwa na Mnyarwanda, Jean Baptiste Mugiraneza.

Mabao mengine mawili ya Azam FC yalifungwa na Kavumbangu dakika ya 45 kwa shuti akimalizia pasi ya Ramadhani Singano ‘Messi’ na dakika ya 63 kwa shuti pia akimalizia pasi ya Mudathir Yahya.

Katika mechi zingine zilizochezwa jana, JKT Ruvu ilipata ushindi wao wa kwanza msimu huu, baada ya kuilaza African Sports mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

No comments:

Post a Comment