KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 5, 2015

TAIFA STARS KUJIPIMA NGUVU NA UNIVERSITY OF PRETORIA

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Jumapili kinatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya University of Pretoria (Tucks FC) jijin Johannesuburg ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Algeria, Novemba 14, mwaka huu jijini Dar es salaam.

Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya progamu ya kocha mkuu, Charles Mkwasa baada ya kufanya mazoezi na vijana wake kwa takribani siku nne mpaka sasa, anahitaji kuona maendeleo ya kikosi chake kabla ya kurejea nyumbani kwa mchezo dhidi ya Mbweha wa Jangwani Algeria.

Stars iliyowasili jijini Johannesburg jumatatu mchana, imefikia katika hoteli ya Holiday Inn Express iliopo katika eneo la Woodmead ambapo imekua ikifanya mazoezi yake asubuhi na jioni katika viwanja vya St. Peters College na kituo cha cha michezo cha Edenvale.

Kuhusu hali ya kambi, kocha mkuu wa Stars Charles Mkwasa amesema anashukru maendeleo ni mazuri vijana wake wote wapo katika hali nzuri hakuna majeruhi na wanaendelea na maaandalizi ya mchezo dhidi ya Algeria utakaopigwa Novemba 14 jijini Dar es salaam.

"Dhumuni la kuweka kambi huku ni kupata nafasi ya kuwaanda vijana kwa mazoezi katika mazingira mazuri ikiwamo viwanja vya mazoezi, chakula na malazi kinachopelekea kuongezeka kwa umakini katika mazoezi" Alisema Mkwasa.

"Tumeanza na mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili kwa wachezaji, nguvu na stamina, pumzi ili kuhakikisha vijana wote wanakua katika kiwango sawa (fitness level) kisha tutaendelea na mazoezi ya kiufundi kwa siku zilizosalia kabla ya kurejea nyumbani" aliongeza Mkwasa.




Wachezaji 26 waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Aishi Manula na Said Mohamed, walinzi ni Shomari Kapombe, Juma Abdul, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Mwinyi Haji, Hassan Isihaka, Salim Mbonde, Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub “Cannavaro”.

Wengine ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudahir Yayha, Salum Abubakar, Said Ndemla, Jonas Mkude, Salum Telela, Farid Musa, Saimon Msuva, Malimi Busungu, Elias Maguri, John Bocco na Mrisho Ngasa.

Aidha wachezaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, wanatarajiwa kuungana na kikosi cha Stars baada ya mchezo wao wa fainali Ligi ya Mabingwa Afrika Jumapili dhidi ya USM Algiers.

NB: Namba ya Afisa Habari wa TFF aliyepo nchini Afrika Kusini +27 78 641 1595.

No comments:

Post a Comment