'
Monday, November 2, 2015
STARS YAENDA AFRIKA KUSINI KUIWEKEA KAMBI ALGERIA
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, kimeondoka leo saa 4 asubuhi kuelekea nchini Afrika Kusini kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mchezo dhidi ya Algeria Novemba 14 jijini Dar es salaam.
Taifa Stars imeondoka kwa usafiri wa Shirika la Ndege la Fastjet ikiwa na kikosi cha wachezaji 24, pamoja na bechi la ufundi linalongozwa na Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa.
Wachezaji waliondoka ni Ally Mustafa, Aishi Manula, Said Mohamed, Juma Abdul, Shomari Kapombe, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Haji Mwinyi, Hassan Isihaka, Salim Mbonde, Kelvin Yondani na Nadir Haroub.
Wengine ni Mudathir Yahya, Frank Domayo, Himid Mao, Salum Abubakar, Farid Mussa, Saimon Msuva, Salum Telela, Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu na John Bocco.
Mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguri anatarajiwa kuungana na kikosi hicho kesho baada ya kuitumikia timu yake katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom leo jumatatu dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Aidha, washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa wanaocheza soka nje ya nchi, wataungana na wenzao baada ya michezo ya mwishoni mwa wikiendi hii.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment