KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 5, 2015

TFF YATAFUTA SULUHU MGOGORO WA ZFA



Kufuatia tishio la Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) la kutaka kuifungia Zanzibar ushiriki wa shughuli za mpira duniani, Rais wa TFF Jamal Malinzi alihitisha kikao cha usuluhishi. 

Kikao hichoi kilikuwa na washiriki toka pande zote za mgogoro ambao ulipelekea mambo ya mpira kupelekwa Mahakamani.

Kikao kimefanyika leo katika Hoteli ya Courtyard Dar Es Salaam chini ya Uenyekiti wa Rais wa TFF,  Jamal Malinzi.

Baada ya kutambua uzito wa suala lenyewe ambalo lingeweza kupelekea Zanzibar kukosa ushiriki michuano ya CAF na CECAFA ili kunusuru soka la Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, kikao kimefikia maamuzi yafuatayo:

1. Uitishwe mkutano mkuu wa Zanzibar Football Association (ZFA) wa dharura kujadili

1.1 Mwenendo wa kamati ya utendaji.

1.2. Mapato na matumizi ya ZFA.

1.3. Kuteua kamati ndogo ya kuandika upya Katiba ya ZFA.

2. Rais wa ZFA, Ravia Idarus, kwa mujibu wa Katiba ya ZFA, ndiye atakeyeitisha mkutano huo.

3. Kamati ya sasa inayoendesha ligi Zanzibar, itaongezewa wajumbe watatu watakoteuliwa na Rais wa ZFA.

Ili maamuzi haya yaweze kuwa na nguvu za kisheria na kikatiba, kikao kimeazimia kuwa mashauri yote yaondolewe Mahakamani sasa na waliohusika kufungua mashtaka hayo wamekubali kuyaondoa mara moja.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linazishukuru pande zote na wadau wote wa Mpira wa Zanzibar waliowezesha kufikia hatua hii muhimu katika maendeleo ya Mpira wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment