KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, April 2, 2015

SIMBA, KAGERA SUGAR DIMBANI J'MOSI



Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika viwanjasita nchini, kwa michezo minne. Michezo miwili itachezwa Jumamosi na michezo mingine miwili itachezwa siku ya Jumapili.

Siku ya Jumamosi, Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, utawaka moto  wakati Kagera Sugar watakapomenyana na Simba SC.

Mjini Tanga, Coastal Union watawakaribisha maafande wa Jeshi la Magereza nchini, Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Ndanda FC ya Mtwara watakuwa wenyeji wa wagonga nyundo, timu ya Mbeya City katika Uwanja wa Nagwanda Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa, Ruvu Shooting wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin ulioko Mlandizi.

Siku ya Jumapili, Stand United watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kambarage huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Polisi Morogoro kwenye Uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.

No comments:

Post a Comment