KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, February 19, 2013

FIFA YAINGILIA KATI UCHAGUZI WA TFF



SHIRIKISHO la Kimataifa la Soka (FIFA), limesimamisha uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uliopangwa kufanyika Februali 24, mwaka huu.


Hatua hiyo imekuja baada ya FIFA kupokea malalamiko ya wagombea walioenguliwa kuwania nafasi katika uchaguzi huo.

Rais wa TFF, Leodger Tenga, alisema jana alipokea simu kutoka FIFA ikitaarifu kusimamishwa kwa uchaguzi huo huku ikitoa taarifa ya kutuma ujumbe wa watu wake kuja nchini kusikiliza madai ya wagombea walioenguliwa.

Tenga alisema ujumbe huo utakuja katikati ya mwezi Machi na itasikiliza malalamiko ya wagombea walioenguliwa, kamati ya uchaguzi na kamati ya rufaa.

Rais Tenga alisema kabla ya kupewa taarifa ya ujio wa wajumbe hao, FIFA ilimuhoji juu ya mwendendo wa mchakato wa uchaguzi huo na maamuzi yaliyotolewa na Kamati ya Rufaa chini ya Mwenyekiti wake Idd Mtinginjola.

Rais Tenga alisema baada ya FIFA kupokea maamuzi ya kamati ya rufaa ilikutana tena juzi na kuamua kuja nchini ili kusikiliza maelezo ya walalamikaji ili haki iweze kutendeka.

Alisema ujio wa FIFA unataka kuja kutenda haki na kuondoa dhana ya wagombea kuonewa na kusema huo utakuwa uamuzi ambao utampa kila mtu haki yake aliyostahili.

"Nimefurahi sana kuona FIFA imeamua kulichukulia jambo hili kwa uzito na kuamua kuja kutoa ufumbuzi na ninaamini baada ya hapo hakuna mtu atakayesema kaonewa kwani kila mtu atapata haki yake," alisema Tenga.

Alisema FIFA imeona bora iepushe vurugu, malumbano yasiyokuwa na msingi ikiwa ni pamoja na kuondoa makundi ambayo yanaweza kuja kuleta athari kubwa kwa soka la Tanzania.

No comments:

Post a Comment