KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, February 20, 2013

HAIJAPATA KUTOKEA-DIAMOND



NGULI wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond' amesema, anajivunia kuweka historia ya kufanya onyesho, ambalo mashabiki wamelipa kiingilio kikubwa ili kumshuhudia.

Diamond ameeleza kupitia mtandao wake kuwa, katika maisha yake, hajawahi kufanya onyesho, ambalo mashabiki walilipa zaidi ya sh. 20,000.

Katika onyesho hilo lililofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa klabu ya Safari Carnival mjini Arusha, kiingilio kilikuwa sh. 150,000 kwa mtu mmoja.

"Kiukweli namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuweza kufanikisha onyesho hilo,"alisema msanii huyo, ambaye amewahi kushinda tuzo kadhaa za muziki za Kilimanjaro.

"Huwezi kuamini, licha ya kiingilio kuwa kikubwa, mashabiki walifurika pasipo hata mimi kutegemea. Kiukweli, ilinifariji sana,"aliongeza.

Kwa mujibu wa Diamond, wingi wa mashabiki hao ulidhihirisha kwamba watanzania wanathamini na kujali vipaji vya wasanii wao tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

"Zamani shoo ya kiingilio kikubwa ilikuwa mpaka msanii atoke nje ya nchi. Hali hii inanipa changamoto ya kuzidi kufanya vizuri, kujituma na kuwa mbunifu zaidi,"alisema.

Diamond alisema moja ya mipango yake ya baadaye kimuziki ni kuitangaza Tanzania kimataifa.

Aliushukuru uongozi wa Safari Carnival na mashabiki wote wa muziki wa Arusha waliojitokeza kushuhudia onyesho hilo.

 

No comments:

Post a Comment