KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, February 10, 2013

AZAM YAIKAMATA YANGA PABAYA


AZAM leo imeikaba koo Yanga baada ya kuibamiza Mtibwa Sugar mabao
4-1 katika mechi ya ligi kuu ya Tanzania Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Manungu uliopo Turiani, Morogoro.

Ushindi huo uliiwezesha Azam kuwa na pointi 33 sawa na Yanga, lakini inazidiwa kwa tofauti ya bao moja la kufunga huku Yanga ikiwa na mchezo mmoja mkononi. Yanga imefunga mabao 29 na kufungwa 12 wakati Azam imefunga mabao 27 na kufungwa 13.

Mshambuliaji Kipre Tchetche ndiye aliyeibeba Yanga baada ya kuifungia mabao mawili kati ya manne. Mabao mengine yalifungwa na Joackisn Atudo na Briany Umony.

No comments:

Post a Comment