KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, February 2, 2013

YANGA YAPUGUZWA KASI NA MTIBWA



YANGA jana ilipunguzwa kasi ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya
Tanzania Bara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, Mtibwa ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa na Shabani
Kisiga na kudumu hadi mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuwapumzisha Athumani Iddi,
Didier Kavumbagu na Frank Domayo na kuwaingiza Hamisi Kiiza, Nurdin
Bakari na Saidi Bahanuzi.

Mabadiliko hayo yaliongeza uhai kwa Yanga, iliyofanikiwa
kusawazisha dakika ya 84 kwa bao lililofungwa na Kiiza baada ya
kuunganisha wavuni krosi kutoka kwa Bahanuzi.

Sare hiyo imeifanya Yanga iendelee kuongoza ligi hiyo kwa kuwa na
pointi 32 baada ya kucheza mechi 15, ikifuatiwa na Azam yenye
pointi 30 na Simba yenye pointi 26.

Katika mechi zingine za ligi hiyo zilizochezwa jana, Mgambo JKT
ilitoka suluhu na Ruvu Shooting wakati Polisi Moro iliichapa
African Lyon bao 1-0.

Simba inatarajiwa kushuka dimbani leo kumenyana na JKT Ruvu kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Coastal Union itamenyana na
Prisons mjini Tanga.

No comments:

Post a Comment