KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, February 3, 2013

STEWART AENDA SUDAN KUSINI




KOCHA Mkuu wa Azam, Stewart Hall amepanga kwenda Sudan Kusini kuwachunguza wapinzani wao, Al Nasir Juba katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Stewart ameieleza tovuti ya klabu hiyo juzi kuwa, anataka kutazama mechi chache za Al Nasir Juba kabla ya timu hiyo kumenyana na Azam.

Al Nasir Juba inatarajiwa kumenyana na Azam mwishoni mwa mwezi huu mjini Dar es Salaam kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Juba.

Stewart alisema ameshawasilisha maombi kwa uongozi wa Azam kutaka aruhusiwe kwenda Juba kwa lengo la kuwapeleleza wapinzani wao.

Kocha huyo raia wa Uingereza alisema anataka kusoma aina ya mchezo wanaocheza Al Nasir Juba ili aweze kukiandaa vyema kikosi chake kukabiliana nao.

“Nimepanga kwenda Sudan hivi karibuni. Kucheza bila kumjua mpinzani wako inakuwa ngumu, nitatumia muda huo kuwajua wapinzani wetu ili kupata picha ya mchezo utakavyokuwa pamoja na kuiandaa timu yangu,” alisema Stewart.

No comments:

Post a Comment