KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, January 10, 2014

KIONGOZI TASWA AFARIKI DUNIA





MWEKA Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na timu ya soka ya chama hicho, Sultan Sikilo amefariki dunia usiku huu katika hospitli ya Rufaa ya Muhimbili, Dar es Salaam.

Katibu wa TASWA, Amir Mhando ameiambia BIN ZUBEIRY usiku huu kwamba, Sikilo alifikishwa hospitali ya Muhimbili, ambako umauti uimfika akitokea hospitali ya Temeke, Dar es Salaam, Alhamisi wiki hii
“Ndugu yetu aligundulika ana matatizo ya homa ya ini siku ya Alhamisi katika hospitali ya Temeke na akahamishiwa Muhimbili, ambako umauti umemfika,”amesema Mhando.

Mhando amesema msiba wa marehemu upo nyumbani kwa wazazi wake Mbagala Maji Matitu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Saa 9:00 Alasiri eneo la Kibada, Kigambni, Dar es Salaam. Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. Amin.

No comments:

Post a Comment