KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 16, 2014

TWIGA STARS WAANZA KAMBI


KIKOSI cha wachezaji 30 wa timu ya soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, kiliingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa kwa mechi yake ya michuano ya Afrika dhidi ya Zambia.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa, wachezaji wa timu hiyo walitakiwa kuripoti kwenye hosteli za shirikisho hilo zilizopo Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Twiga Stars na Zambia, zinatarajiwa kumenyana mwezi ujao katika mechi ya kwanza ya mchujo ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wanawake, zitakazofanyika baadaye mwaka huu nchini Namibia.
Kwa mujibu wa Wambura, mechi ya awali kati ya timu hizo itachezwa mjini Windhoek, Namibia na ya marudiano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji walioitwa kwenye kikosi hicho na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rogasiun Kaijage ni Amina Ally (Lord Baden Sekondari), Amisa Athuman (Marsh Academy), Anastazia Anthony (Lord Baden Sekondari), Asha Rashid (Mburahati Queens), Aziza Mwadini (Zanzibar) na Belina Julius (Lord Baden Sekondari).
Wengine ni Donisia Daniel (Lord Baden Sekondari), Esther Chabruma (Sayari Queens), Evelyn Sekikubo (Kwimba Chuoni), Fatuma Bushiri (Simba Queens), Fatuma Hassan (Mburahati Queens), Fatuma Issa (Evergreen) na Fatuma Mustapha (Sayari Queens).
Wachezaji wengine ni Fatuma Omari (Sayari Queens), Happiness Hezron (Copa Coca-Cola Ilala), Maimuna Hamisi (U20 Tanzanite), Maimuna Said (JKT), Mwajuma Abdallah (Real Tanzanite), Mwapewa Mtumwa (Sayari Queens), Najiat Abbas (Makongo Sekondari) na Neema Paul (U20 Tanzanite).
Wengine ni Pulkeria Charaji (Sayari Queens), Semeni Abeid (Real Tanzanite), Shelder Boniface (Makongo Sekondari), Sophia Mwasikili (Sayari Queens), Theresa Yona (TSC Academy), Vumilia Maarifa (Evergreen) na Zena Khamis (Mburahati Queens).

No comments:

Post a Comment