KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, January 4, 2014

MKWASA AANZA KIBARUA YANGA





Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara timu ya Young Africans leo imeeanza kujifua katika viwanja vya bora Mabatini Kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa.

Young Africans ilisimama kufanya mazoezi kwa siku takribani tatu kufuatia kufanya mabadiliko ya benchi la Ufundi na leo rasmi imeanza mazoezi asubuhi chini ya makocha wasaidzi Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali.

Mkwasa alitumia muda wa dakika 5 kuongea na wachezaji wote waliofika mazoezini siku ya leo, kuwaelekeza nini wanapaswa kufanya na kuzingatia mafunzo yake ambapo wachezaji waliweze kutekeleza kwa kiwango cha hali ya juu.

Kocha wa makipa Juma Pondamali aliwafua vilivyo magolikipa Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida" na kusema huu ni mwanzo tu kwani anaamini wachezaji hao watakua katika kiwango kizuri kutokana na uwezo wanaouonyesha katika mazoezi anayaowapatia.

Kikosi cha Young Africans kesho kitaendelea na mazoezi asubuhi katika uwanja wa Mabatini Kijitonyama ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili na mashindano ya kimataifa.

Aidha washambuliaji Hamis Kiiza na Emmanuel Okwi waliokwenda kwao nchini Uganda kwa ajili ya matatizo ya kifamilia wanatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki tayari kuungana na wenzao kujiandaa na mzunguko wa pili.

Uongozi wa Young Africans SC umepata warithi wa nafasi tatu za benchi la ufundi (Charles Boniface Mkwasa, Juma Pondamali na Dr. Suphian Juma), huku wakiendelea na mchakato kumpata kocha mkuu ambaye atachukua nafasi ya mholanzi Ernie Brandts aliyesitishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.

Charles Boniface Mkwasa "Master" aliyekua kocha mkuu wa timu ya Ruvu Shooting katika mzunguko wa kwanza anachukua nafasi ya aliyekua kocha msaidizi Fred Felix "Minziro" ambaye muda wake umemalizika mwishoni mwa mwaka 2013.

Mkwasa ambaye aliichezea Young Africans miaka ya 80's kwa kiwango cha hali juu pia alishawahi kuwa Kocha Mkuu/Msaidizi kwa kikosi cha Jangwani kwa vipindi tofauti jambo ambalo linamfanya aiwe mgeni katika mitaa ya Twiga na Jangwani.

Kocha wa makipa wa timu ya Taifa Tanzania "Taifa Stars" Juma Pondamali "Mensah" anachukua nafasi ya aliyekua kocha wa makipa mkenya Razaki Siwa ambaye pia alistishiwa mkataba wake mwishoni mwa mwaka 2013.

Pondamali golikipa aliyeichezea Yanga miaka ya 80's kwa kwa kiwango cha hali ya juu hata kufikia kuwa katika kikosi cha Tanzania kilichoshiriki mashindano ya Mataifa Afrika nchini Nigeria mwaka 1980, sio mgeni katika timu ya Young Africans kwani awali alishwahi kuwa kocha msaidizi kwa vipindi tofauti.

Dr Suphian Juma anachukua nafasi ya Dr Nassoro Matuzya ambaye pia alisitishiwa ajira yake mwishoni mwa mwaka 2013 pamoja benchi la Ufundi.

No comments:

Post a Comment