KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 3, 2014

CHUJI AJIPELEKA AZAM


KIUNGO wa zamani wa klabu za Simba na Yanga, Athumani Iddi 'Chuji' jana alionekana akifanya mazoezi na wachezaji wa Azam kwenye uwanja wa Azam Complex ulioko Mbagala, Dar es Salaam.

Kuonekana kwa Chuji kwenye kikosi cha Azam kulitafsiriwa kuwa, huenda amejiunga na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.

Hata hivyo, Msemaji wa Azam, Jaffer Iddi amesema leo kuwa, Chuji ameomba kufanya mazoezi na timu hiyo kwa ajili ya kujiweka fiti.

Alisema jukumu la kusajili wachezaji ni la kocha mkuu wa timu hiyo, hivyo iwapo atamuona anafaa kusajiliwa, anaweza kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment