KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 3, 2014

MAXIMO AMPA MASHARTI MAZITO MANJI

KOCHA Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo akizungumza na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji leo makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Maximo amemweleza Manji kuwa lazima timu hiyo ifanye mazoezi kwenye Uwanja wa Kaunda, badala ya kutumia viwanja vingine kwa kuazima.

Kocha huyo pia alimweleza Manji kuwa lazima ahakikishe vyumba vyote vya wachezaji vilivyoko kwenye makao makuu ya klabu hiyo vinakuwa na kipoza hewa na viwekwe tiles ili kuvifanya viwe na hadhi badala ya vilivyo hivi sasa.

Wengine pichani ni Katibu Mkuu wa Yanga, Benno Njovu na Ofisa Habari, Baraka Kaziguto.

No comments:

Post a Comment