KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, September 7, 2012

SIMBA YAWAHUZUNISHA MASHABIKI WAKE

MASHABIKI wa klabu ya Simba jana waliondoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakiwa vichwa chini huku wakiwa na huzuni kubwa baada ya kushuhudia timu yao ikichapwa mabao 3-0 na Sofapaka ya Kenya.

Mashabiki hao walifurika kwa wingi uwanjani wakiwa na hamu kubwa ya kuwaona nyota wao wapya, Daniel Akuffo kutoka Ghana, Paschal Ochieng kutoka Kenya na Komabil Keita kutoka Mali, lakini mambo yalikwenda kombo.

Tatizo kubwa lililojitokeza kwenye kikosi cha Simba ni safu yake ya ulinzi kushindwa kucheza kwa uelewano, ambapo Ochieng alionekana wazi kuwa mzito wakati Keita hakuwa makini katika kuokoa mipira.

Mshambuliaji wa zamani wa Yangam John Barasa alikuwa mwiba kwa mabeki wa Simba baada ya kuifungia Sofapaka mabap mawili kati ya matatu.

Alifunga bao la kwanza kwa njia ya penalti baada ya Keita kuunawa mpira kwa makusudi ndani ya eneo la hatari na kuonyeshwa kadi ya njano.

Simba ilipata pigo dakika ya 40 wakati Akuffo alipoumia na kutolewa nje baada ya kukanyagwa kifuani na beki mmoja wa Sofapaka. Nafasi yake ilichukuliwa na Abdalla Juma.

Mabao mengine ya Sofapaka yalifungwa na Barasa dakika ya 55 na George Nyaga dakika ya 66.

Simba SC; Juma Kaseja (1), Shomary Kapombe (15), Amir Maftah (17)/Paul Ngalema, Paschal Ochieng (5), Komabil Keita (4)/Juma Nyosso, Mwinyi Kazimoto (14), Salim Kinje/Ramadhani Chombo (12)/, Haruna Moshi (3)/Kiggi Makassy, Edward Christopher (19)/Nassor Masoud, Daniel Akuffo (13)/Abdallah Juma na Mrisho Ngassa (16).

Sofapaka FC; Duncan Ochieng (39), Anthony Kimani (11), James Situma (14), Edgar Ochieng (5), George Owino (26), Collins Okoth (45), Osborne Monday (2)/Thomas Wanyama, Danson Kago (13)/Hashimu Mukwana, Joseph Nyangit (30), Humphrey Mieno (20)/Robert Binja na John Baraza.

No comments:

Post a Comment