KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, September 15, 2012

ZANTEL YAINGIA MKATABA NA AFRICAN LYON

Ofisa Mkuu wa Biashara wa Zantel, Sajid Khan akimkabidhi jezi, Mkurugenzi wa Michezo, Leonard Thadeo kwa niaba ya klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam, katika hoteli ya Hyatt Regency (zamani Kilimanjaro), Dar es Salaam wakati wa kutangaza kuingia mkataba wa kudhamini klabu hiyo kwa miaka mitatu. Wanaomfuatia Thadeo ni Meneja Mkuu wa African Lyon, Rahim Kangezi ‘Zamunda’ na Charles Otieno, Mkurugenzi wa Ufundi wa African Lyon. Kulia kabisa ni mchezaji chipukizi wa Lyon, Jarufu Magesa, ambaye anapelekwa na klabu Marekani kusoma. Lyon itashuka dimbani jioni hii kumenyana na Simba SC katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
CHANZO CHA HABARI: BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment