
SIMBA leo imefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuicharaza Azam FC mabao 3-2 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa michuano ya ligi kuu ya Tanzania Bara, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi.
Ushindi huo ulikuwa wa kulipiza kisasi kwa Simba kufuatia kuchapwa mabao 3-1 na Azam katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Kagame.
Azam ilikuwa ya kwanza kupata mabao kupitia kwa John Bocco na Kipre Tchetche kabla ya Daniel Akuffour kuifungia Simba bao dakika chache kabla ya mapumziko na kuyafanya matokeo yawe 2-1.
Simba ilibadili mchezo kipindi cha pili na kufanikiwa kusawazisha kwa bao lililofungwa na Emmanuel Okwi kabla ya Mwinyi Kazimoto kuongeza la tatu na la ushindi.
No comments:
Post a Comment