KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 13, 2012

UCHE IWUJI: SINA UJA UZITO

LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu machachari wa kike wa Nollywood, Uche Iwuji amekanusha madai kuwa ana uja uzito.
Akizungumza na mtandao wa Nigeriafilms wiki hii, Uche alisema madai hayo hayana ukweli wowote na ni ya kupika.
Uche alisema anashangazwa na tabia ya baadhi ya watu, ambao wamekuwa wakizusha vitu vingi ambavyo si vya kweli juu yake.
"Inanishangaza kwamba anatokea mtu mmoja na kupika stori kuhusu mimi kwamba nina uja uzito, kitu ambacho ni uongo ulio wazi,"alisema mwigizaji huyo mwenye sura na umbo lenye mvuto.
"Sina uja uzito na hata kama ningekuwa nao, ni kitu ambacho siwezi kukificha,"alisisitiza.
Uche amekuwa akiandamwa mara kwa mara na tuhuma mbali mbali, lakini amekuwa akipambana nazo na kuendelea kufanya vizuri kwenye fani.
Kwa sasa, msanii huyo yupo nchini Uingereza, ambako amekwenda kwa mapumziko na mara baada ya kurejea Nigeria, anatarajia kutengeneza filamu yake ya kwanza.
"Labda taarifa sahihi kuhusu mimi ni kwamba kwa sasa najaribu kutengeneza filamu yangu mwenyewe,"alisema.

No comments:

Post a Comment