KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 20, 2012

DAIMOND: MIMI NA WEMA BASI


BAADA ya kuficha ficha kwa muda mrefu, hatimaye msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Naseeb Abdul 'Diamond' ameamua kufunguka na kuweka wazi kuwa, hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Wema Sepetu.
Diamond amesema kwa sasa Wema ana mchumba wake wanayependana na anamuheshimu mtu huyo kama shemeji yake.
Kwa mujibu wa Diamond, uhusiano wake na Wema kwa sasa ni sawa na mtu na dada yake kwa sababu bado wanaheshimiana.
Diamond ameeleza hayo wiki hii kupitia tovuti yake mpya, baada ya kuwepo na taarifa zenye utata kuhusu uhusiano wake na Wema
Wasanii hao wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu kiasi cha kufikia hatua ya kutaka kufunga ndoa, kabla ya ndoa hiyo kuparaganyika.
"Najua watu wengi sana mnavutiwa na uhusiano wetu na furaha yenu ni kutuona sisi wawili tukiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi," ameeleza Diamond kupitia tovuti yake hiyo.
"Na mmekuwa mkifurahishwa sana na stori za hapa na pale kuhusu sisi. Mkiskia kuwa wawili sisi tupo pamoja na hata pindi mkituona tuko pamoja, mmekuwa mkishangilia na kufurahi. Lakini ukweli ni kwamba, mimi na Wema hivi sasa si wapenzi tena," aliongeza Diamond, ambaye tovuti yake hiyo imepata wasomaji zaidi ya lakini tatu hadi sasa.
Akifafanua, Diamond alisema kwa sasa yeye na Wema ni marafiki wa kawaida, ambao wanashirikiana katika kazi mbali mbali za sanaa na zilizo nje ya sanaa katika harakati za kujenga taifa la Tanzania.
"Ni vizuri mngependa kufahamu kwamba, Wema ana mpenzi wake, ambaye namfahamu na tunaheshimiana kama mtu na shemeji yake. Huo ndio ukweli kuhusu mimi na Wema,"alisisitiza.
Msanii huyo nyota wa kizazi kipya alisema, ameandaa kazi tofauti tofauti za sanaa alizozifanya na Wema na zinatarajiwa kuingia sokoni hivi karibuni.
Katika hatua nyingine, Diamond amesema wacheza shoo wake wapo mapumzikoni nchini Marekani kwa muda mfupi na wanatarajiwa kurejea nchini hivi karibuni.
Diamond alisema ameamua kuwapumzisha wacheza shoo hao kwa muda baada ya kufanya nao kazi ngumu kwa kipindi kirefu na iliyozaa matunda.
"Nimewapeleka huko ili waweze kurifreshi akili zao na miili yao kwa sababu wamefanyakazi kwa muda mrefu sana,"alisema Diamond.

1 comment:

  1. This is my primary dribble to dissipate this website. I begin numerous remarkable chapters likewise I vim pain to the cancer of my blog. Celebrate for sharing beneficial information. general electric appliances

    ReplyDelete