KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 13, 2012

TBL YAIPONGEZA SIMBA

KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia Bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager ambayo ni mdhamini wa vilabu vya Simba na Yanga, imeipongeza Simba kwa kutwaa Ngao ya Jamii mara mbili mfululizo na kusema ni ishara nzuri ya matokeo mengine mazuri katika ligi kuu inayotarajiwa kutimua kivumbi Jumamosi hii.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe, alisema: “Tumefurahishwa sana kwa ushindi huu wa Simba kwani ni ishara kuwa wamepania kutetea ubingwa wao vilivyo msimu huu.”

Alisema mchezo wa Simba dhidi ya Azam ulikuwa mkali na wenye ushindani mkubwa lakini Simba ilionyesha uwezo mkubwa na kweza kuibuka na ushindi wa mabao 3-2.

“Siku zote sisi kilimanjaro Premium Lager tunajihusisha na ushindi na ndio maana tumepania kuifikisha Soka ya Tanzania katika kilele cha mafanikio,” alisema Kavishe na kuongeza kuwa nia yao kama wadhamini ni kuendelea kuona timu hizi zinafanya vizuri katika ligi kuu na mashindano mengine yakiwemo ya kimataifa.

Katika taarifa yake Meneja huo alitoa rai kwa timu ya Yanga pia kuhakikisha iaanza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya Prisons vizuri huko Mbeya wakati Simba itamenyana na African Lyon Jijini Dar es Salaam.

“Tunatumai kuwa timu hizi, zinazodhaminiwa na Bia yetu ya Kilimanjaro Premium Lager, zitaonyesha nidhamu ya hali ya juu wakati wa ligi hii na kuleta ushindani mkubwa kama ilivyo miaka yote,” alisema Kavishe.

Bia ya Kilimanjaro Premium Lager inatarajiwa kukabidhi mabasi ya kisasa kwa timu hizi mbili hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment