KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, September 5, 2012

PENDO NDIYE MISS MWANZA 2012

MREMBO Pendo Simon mwishoni mwa wiki iliyopita alitawazwa kuwa mrembo wa mkoa wa Mwanza, 'Redds Miss Mwanza 2012' katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Yatch Club mjini hapa.
Pendo alitwaa taji hilo baada ya kuwabwaga warembo wenzake 13 na hivyo kujinyakulia kitita cha sh. 500,000 na televisheni yenye ukubwa wa inchi 24.
Katika shindano hilo lililohudhuriwa na mashabiki lukuki, Happiness Daniel alishika nafasi ya pili wakati Stella Augustino aliibuka mshindi wa tatu.
Kufuatia kushika nafasi hizo,Happiness alizawadiwa sh. 300,000 na dekoda wakati Stella alizawadiwa sh. 200,00 na dekoda.
Washiriki wengine waliofuzu kuingia hatua ya tano bora ni Aisha Eddy na Clara Nuru, ambao walizawadiwa sh. 100,000 na sh. 50,000.
Katika shindano hilo, washiriki walichuana kwa mavazi ya ufukweni, ubunifu na kutokea matembezini nyakati za jioni.
Mgeni rasmi katika shindano hilo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga.
Katika hatua nyingine, warembo 11 wameingia kambini mjini Arusha kwa ajili ya shindano la kuwania taji la mrembo wa Kanda ya Kaskazini.
Shindano hilo limepangwa kufanyika keshokutwa kwenye hoteli ya Naura Spring iliyopo mjini Arusha.
Mratibu wa shindano hilo, Emma Mroso alisema juzi kuwa, maandalizi ya shindano hilo yanaendelea vizuri.
Aliwataja warembo watakaowania taji hilo kuwa ni Mishi Mziray, Dalina Hashim, Anita Mboya, Highmanna Lyimo, Anande Radhiel, Waridi Frenk, Buya Ernest, Lucy Stephano, Neyla Hashim, Trovina Mpanda na Theresia Kimolo.

No comments:

Post a Comment