MASHINDANO ya urembo Kanda ya Temeke "Redd's Miss Temeke" linafanyika Sept 21, mwaka huu katika ukumbi wa PTA( SabaSaba Hall), likiwashirikisha warembo 15 kutoka vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe.
Warembo hao ambao wamekuwa wakijifua kwa takriban wiki mbili sasa, chini ya ukufunzi wa Leyla Bhanji na Dickson Daud kutoka THT kwa upande wa shoo, wanawania nafasi tatu za kupata tiketi ya moja kwa kwenye shindano la taifa, Redd's Miss Tanzania itakayofanyika baadaye mwaka huu.
Shindano hilo, litakuwa na burudani ya bendi sanjari na muongozaji maarufu katika sanaa nchini ambaye atakuwa mahsusi kuongeza burudani ya mashabiki kupata kile wanachotarajia. Temeke imewahi kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Magesse aka Millen mwaka 2001, Sylvia Remmy Bahame mwaka 2003 na Genevieve Mpangala.
Lakini pia imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka.
Mbali kinywaji cha Redd's, Miss Temeke 2012 pia imedhaminiwa na Kampuni ya gazeti la Jambo Leo, Dodoma Wine, Push Mobile, City Sports Lounge, katejoshy.blogsport.com GlobalPublishers kupitia magazeti yake pendwa,100.5 Times FM, Kitwe General Traders, Mariedo Boutique na 88.4 Clod's FM.
Warembo wanaendelea na mazoezi na Jumamosi itaongezeka safu ya wakufunzi akiwemo Miss Temeke 2002, Regina Mosha na Miss Temeke 2003, Hawa Ismail na kutoa uzoefu wao na jinsi walivyofanikiwa katika fani hiyo na kuwapa uzoefu wao katika mashindano ya urembo.
Benny Kisaka
Mkurugenzi
BMP Promotions
No comments:
Post a Comment