KLABU ya Real Madrid ya Hispania imefanikiwa kumnasa kiungo Michael Essien kutoka Chelsea ya England.
Awali, kiungo huyo wa kimataifa wa Ghana pia alikuwa akiwaniwa na Arsenal ya England, ambayo ilikuwa ya kwanza kuwasilisha maombi ya kumsajili.
Essien hakucheza juzi wakati Chelsea ilipomenyana na Atletico Madrid ya Hispania katika mechi ya michuano ya Kombe la UEFA Super na kuchapwa mabao 4-1.
Kocha Mkuu wa Chelsea, Roberto de Matteo alithibitisha kabla ya mechi hiyo kuwa, Essien alikuwa katika mipango ya kuihama kwa muda klabu hilo.
Baadaye, Chelsea ilitoa taarifa iliyothibitisha kuwa, Essien amejiunga na Real Madrid kwa mkopo wa muda mrefu.
Essien (29), ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2005 akitokea Lyon ya Ufaransa, sasa ataungana na kocha wake wa zamani, Jose Mourinho, ambaye ndiye aliyempeleka Stamford Bridge.
No comments:
Post a Comment