KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, September 15, 2012

TAMASHA LA SERENGETI FIESTA LAFANA DODOMA

Msanii anayetamba katika miondoko ya R&B hapa bongo, Ben Paul akiwarusha wakazi wa mji wa Dodoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta lililofanyika jana usiku kwenye uwanja wa Jamhuri.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah kutoka THT akitumbuiza jukwaani wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 mjini Dodoma.

Anaitwa Recho kwa jina la kisanii kutoka nyumba ya vipati THT,akiimba jukwaani kwa madaha kabisa.

Msanii Rich Mavoko akiwapagawisha mashabiki wakati wa tamasha hilo


Msanii wa bongofleva aitwaye Shetta akiwaimbisha washabiki wake


Mmoja wa wasanii chipukizi katika anga ya muziki wa kizazi kipya,ambaye pia aliibuliwa na shindano la Serengeti Supa Nyota kutoka jijini Mwanza, aitwaye Young Killer akikamua jukwaani mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Dodoma.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa amebebwa juu mara baada ya kujitokeza jukwaani na wasanii waliopa mtafu kutoka THT.

No comments:

Post a Comment