KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 13, 2012

KASEJA AMKINGIA KIFUA OCHIENG

NAHODHA wa Simba, Juma Kaseja amemkingia kifua beki Paschal Ochieng kutoka Kenya na kuwataka mashabiki wa timu hiyo kumpa muda kwa vile bado hajazoea mfumo wa uchezaji wa timu hiyo.
Kaseja alisema hayo juzi mara baada ya Simba kuicharaza Azam mabao 3-2 na kutwaa Ngao ya Jamii katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Wakati wa mechi hiyo, mashabiki wa Simba walikuwa wakipiga kelele kuonyesha hawaridhishwi na uchezaji wa Ochieng kutokana na kuwa mzito katika kutoa maamuzi.
Kaseja alisema Ochieng ni beki mzuri, hivyo anahitaji kupewa muda ili kuzoeana na wenzake na kuongeza kuwa, ana imani atakuwa mtu muhimu kwa Simba.
Alisema makosa yaliyofanywa na beki huyo wa zamani wa Yanga wakati wa mechi hiyo ni ya kibinadamu kwa vile hakuwa na mawasiliano mazuri na beki mwenzake wa kati, Shomari Kapombe.
Kipa huyo namba moja nchini alisema makosa hayo ndiyo yaliyoiwezesha Azam kupata mabao mawili katika kipindi cha kwanza, lakini mambo yalibadilika baada ya kufanyika kwa mabadiliko katika kipindi cha pili.
"Ochieng alikuwa bado ana wakati mgumu na hii ni mara ya pili kucheza hapa uwanja wa Taifa baada ya mchezo kati yetu na Sofapaka, nawaomba mashabiki wa Simba wampe nafasi, atafanya vyema, hata wachezaji wengine wageni wavumiliwe kwanza, watazoea,"alisema kipa huyo.

No comments:

Post a Comment