KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 13, 2012

SINA HARAKA YA KUOLEWA-BIMBO

LAGOS, Nigeria
BAADA ya ukimya wa muda mrefu kuhusu maisha yake binafsi, mcheza filamu nyota wa Nollywood, Bimbo Akintola ameibuka na kusema kuwa hana haraka ya kuolewa.
Bimbo, ambaye alijitosa kwenye fani hiyo miaka kadhaa iliyopita, alisema wiki hii kuwa, suala la kufunga ndoa ni zito na hutokea kutokana na mipango ya Mungu.
"Ndoa ni suala zito na sina haraka ya kulifikia.Huo ndio ukweli ulivyo,"alisisitiza mwanadada huyo machachari kwa filamu za mapenzi.
Bimbo ameripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na nyota kadhaa wa filamu pamoja na wanaume wengine nje ya fani hiyo.
"Nakaribia kutimiza umri wa miaka 37, bado sijaolewa na naweza kuendelea hivi kama sintampata mwanaume sahihi wa kuniona,"alisema mama huyo.
"Sisi sote tupo duniani kama watu pweke. Baadhi yetu wataolewa, baadhi yetu hawataolewa. Baadhi yetu watakuwa na watoto, wengine hawatakuwa nao. Hivyo kamwe siwezi kujihukumu kulingana na maisha ya wengine,"alisisitiza mwanamama huyo.
Bimbo alikiri kuwa, aliwahi kutaka kufunga ndoa na wapenzi wake wawili wa zamani, lakini aliwatolea nje baada ya kubaini kuwa, hawataweza kumfaa katika maisha yake.
"Kama ningetaka kuolewa zaidi ya mara 15, ningeweza kufanya hivyo. Lakini siwezi kufunga ndoa kwa ajili ya watu, nitafunga ndoa kwa ajili yangu. Kama nitampata mtu atakayenifanya nijihisi naweza kufunga ndoa, nipo tayari kufanya hivyo," alisisitiza mwanamama huyo.

No comments:

Post a Comment