KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, September 5, 2012

MISS UTALII MWENYE KIPAJI KUSAKWA KESHO

WAREMBO wanaowania mataji ya Miss Utalii katika kanda za Ilala na Kinondoni, kesho watachuana kuwania taji la mrembo mwenye kipaji.
Mratibu wa shindano hilo, Yelemia Mayenga alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, warembo hao watachuana kuanzia saa mbili usiku kwenye hoteli ya Lamada.
Yelemia alisema shindano la vipaji ni hatua ya awali katika kusaka warembo wa kanda hizo, katika shindano linalotarajiwa kufanyika Septemba 14 mwaka huu kwenye hoteli hiyo.
Alisema kiingilio katika shindano la kesho kinatarajiwa kuwa sh. 20,000 kwa VIP na sh. 10,000 kwa viti vya kawaida.
Mratibu huyo alisema shindano hilo litapambwa kwa burudani kutoka bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia na kikundi cha taarab cha T-Moto.
Yelemia alisema siku ya fainali ya shindano hilo, kiingilio kitakuwa sh. 30,000 kwa VIP na sh. 20,000 kwa viti vya kawaida.
Shindano hilo limedhaminiwa na hoteli ya Lamada, Rashid Sports Entertainments, Mzee Yusuph Enterprises, Zizzu Fashion, Essy Media, Pandisha Import, Tambaza Court Broker and Action Mart na Dar es Salaam City Collage.
Wadhamini wengine ni Geita Gold Mine Limited,Travertine Hotel, Eriado Point View, Stanford Bridge Institute of Journalism, Community Development and Business Studies, Times Radio 100.5 FM, Uhuru FM, Gabriel Designer na Hameed
Designer
.

No comments:

Post a Comment