KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, September 7, 2012

AY BALOZI MPYA WA AIRTEL

Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa kumtambulisha AY (kushoto), makao makuu ya Airtel, Morocco, Dar es Salaam leo. Kulia ni Hawa Bayumi, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel.

Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akimkabidhi simu AY (kushoto), makao makuu ya Airtel, Morocco, Dar es Salaam leo. Kulia ni Hawa Bayumi, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel.


MWANAMUZIKI nyota Tanzania, Ambwene Yessayah ‘AY’ ameteuliwa kuwa Balozi wa Airtel, akimpokea Ally Kiba aliyekuwa balozi wa kampuni hiyo msimu uliopita.

Meneja Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando amesema leo kwamba wameamua kumpa dili hiyo AY baada ya kuvutiwa na kazi zake kwa ujumla, akiwa msanii ambaye ametwaa tuzo kibao za kitaifa na kimataifa na kushirikiana na wanamuziki wengi wa kimataifa sambamba na kutumbuiza katika maonyesho makubwa hadi Ulaya na Amerika.

Kwa upande wake AY, alishukuru kwa dili hilo na kusema Airtel hawatajuta kwa kufanya naye kazi. Kwa kuanzia, AY alisema atafanyia kazi mradi wa kuchangia elimu ambao Airtel inashirikiana na BAMVITA.

Amewataka Watanzania kuchangia mradi huo kwa kutuma neno “Vitabu” kwenda namba 15626 na wataweza kuchangia Sh. 200 katika mradi huo au wengine kuchangia kwa Airtel Money kupitia namba 0788 041361.

AY pia alikabidhiwa simu aina ya Samsung Galaxy Tab7.0 Plus yenye thamani ya Sh. 1.200,000 na Mmbando, sambamba huduma zote ambazo zinalipiwa na Airtel.

Naye Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi alisema wanampokea kwa furaha AY na wanaamini watashirikiana naye vema kufanya kazi za kijamii za kampuni hiyo.

No comments:

Post a Comment