KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, September 13, 2012

BEN POL HATAKI KOLABO

MKALI wa miondoko ya R&B, Ben Pol amesema kwa sasa hana mpango wa kufanya kolabo na msanii yeyote wa muziki wa kizazi kipya nchini.
Pol alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, kufanya kolabo kumekuwa kukichelewesha mipango yake ya kutengeneza albamu.
Msanii huyo, ambaye kwa sasa anatamba na singo yake ya Maneno maneno alisema, ataendelea kufanya kolabo baada ya matayarisho ya albamu yake kukamilika.
Kwa mujibu wa Pol, albamu yake mpya itajulikana kwa jina la Pete na itakuwa na vibao sita, ambavyo amevitunga na kuviimba peke yake.
"Unajua, ukijikita kwenye kazi za wasanii wenzako, unatumia muda mwingi na matokeo yake wenzako wanakamilisha albamu zao za kwako zinalala,"alisema.
Aliongeza: "Hii ndiyo sababu iliyonifanya nisihiriki katika kazi ya msanii yeyote kwa sasa. Mtaniwia radhi kwa wale, ambao nitakuwa nimewakwaza kwa uamuzi huu, tuvumiliane, nitakapomaliza nitashiriki tu,” alisema Pol.
Vibao vingine vya msanii huyo vinavyotamba kwa sasa ni pamoja na Nikikupata, Samboira, Pete na Yatakwisha, alichomshirikisha Linah.

No comments:

Post a Comment