KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 4, 2012

Bongo Star Search kuanza ziara kusaka vipaji mikoani

ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star
Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika ukumbi wa Royal
Village.
Akizungumzia ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark
Production, Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika
ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.
Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano
kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia
Dar es salaam.
Alisema kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa
kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa
kuimba aina zote za nyimbo.
“ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata
kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa
mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo,” alisema Ritha.

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay.

No comments:

Post a Comment