KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 11, 2012

Stars, Gambia zaingiza mil 124/-

Mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa
Stars) na Gambia (The Scorpions) iliyochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 124,038,000.

Mapato hayo yametokana na washabiki 31,122 waliokata tiketi kushuhudia
pambano hilo kwa viingilio vya sh. 3,000, sh. 5,000, sh. 10,000, sh. 20,000
na sh. 30,000.

Washabiki 25,901 walikata tiketi za sh. 3,000. Asilimia 18 ya mapato hayo ambayo ni sh. 18,921,050.85 ilikwenda kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wakati gharama kabla ya mgawo zilikuwa tiketi (sh. 6,555,000), bonasi kwa Taifa Stars (sh. 15,767,542.37), waamuzi
(sh. 13,372,000), usafi na ulinzi (sh. 2,350,000), maandalizi ya uwanja- pitch
preparation (sh. 400,000), Wachina- Beijing Construction (sh. 2,000,000),
umeme (sh. 300,000) na mafuta ya jenereta (sh. 200,000).

Kwa upande wa mgawo asilimia 20 ya gharama za mechi ni sh. 12,834,481,
asilimia 10 ya uwanja sh. 6,417,241, asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) sh. 3,208,620, asilimia 20 ya Mfuko wa Maendeleo ya
Mpira wa Miguu (FDF) sh. 12,834,481 na asilimia 45 ya TFF (sh. 28,877,583).

No comments:

Post a Comment