KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, June 30, 2012

WINFRIDA ASHINDA TAJI LA MISS UNIVERSE TANZANIA 2012



MREMBO Winfrida Dominic (19) wa Dar es Salaam ameshinda taji la Miss Universe Tanzania, baada ya kuwashinda washiriki 16 katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam.
Pamoja na ushindi huo, Winfrida alipata ushindani mkali hasa katika hatua ya tano bora, ambapo warembo walijibu maswali mbalimbali kabla ya kutangazwa mshindi.
Winfrida, alionekana kujiamini tangu mwanzo wa mashindano hayo, na hiyo kuwa silaha kubwa katika mafanikio yake. Uzuri wake wa asili pia ulichangia kupata ushindi na kupata tiketi ya kuiwakilishaTanzania katika mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika Desemba katika nchi itakayotangazwa baadaye.
Mbali na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, mrembo huyo pia alizawadiwa sh. milioni 3, na kupewa ofa ya kwenda kusoma nchini Marekani katika Chuo cha New York Film Academy.
"Ndoto yangu imetimia, nilipoamua kushiriki katika mashindano haya, lengo langu lilikuwa ushindi, ushindani ulikuwa mkubwa sana na hasa hatua ya tano bora, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kushinda taji hili," alisema Winfrida.
Nafasi ya pili katika mashindano hayo ilikwenda kwa Bahati Chando (20), pia wa Dar es Salaam, ambaye alipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth na kuzawadiwa kitita cha sh milioni 1, huku Dorice Mollel (21) akiibuka katika nafasi ya tatu na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Tourism Queen International na kitita cha sh 500,000.
Dar es Salaam ilitawala mashindano hayo, kwani hata nafasi ya nne na tano zilichukuliwa na Kundi Mligwa (23) na Lilian Kolimba, ambao walizawadiwa sh 100,000 kila mmoja

No comments:

Post a Comment