KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 11, 2012

Extra Bongo kupamba tuzo za TASWA

BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo itatumbuiza katika sherehe za utoaji
wa tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2011 zinazoandaliwa na Chama
cha Waandishi wa Habari za Michezo Nchini (TASWA).
Sherehe hizo zinatarajia kufanyika keshokutwa katika Ukumbi wa Diamond
Jubilee ambapo wanamichezo wa michezo mbalimbali watawania tuzo hizo
ambazo zimedhaminiwa na Kampuni ya Bia ya Srengeti (SBL).
Meneja Masoko wa SBL, Iman Lwinga, alisema maandalizi kwa ajili ya sherehe
hizo yanaendelea vizuri na kampuni yake imejipanga kuhakikisha sherehe za
utoaji tuzo hizo zinakuwa na mafanikio.
Mshindi wa jumla katika tuzo hizo atajinyakulia kitita cha sh. milioni 12 na
pamoja na cheti na kikombe wakati washindi wengine wa kila mchezo
watajinyakulia kitita cha shilingi milioni moja.
Wanamichezo wanaowania tuzo hizo upande wa mpira wa miguu wanawake
ni Mwanahamisi Omary na Asha Rashid (Mburahati Queens), Fatuma
Mustapha(Sayari) na Etoe Mlenzi (JKT) wakati wanaume ni John Bocco na
Aggrey Morris(Azam) na Juma Kaseja (Simba).
Tuzo ya wanamichezo bora wanaocheza kwa upande wa soka nje ni Henry Joseph, Mbwana Samatta na Sophia Mwasikili wakati tuzo ya mchezaji bora chipukizi inawaniwa na Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars), Shomari Kapombe na Salum Abubakar na mchezaji wa nje anayecheza nchini ni Haruna Niyonzima (Yanga), Kipre Tchetche (Azam) na Emmanuel Okwi (Simba).
Kwa upande wa mchezo wa kikapu kwa wanawake ni Doritha Mbunda na
Evodia Kazinja (JKT Queens) na Faraja Malaki (Jeshi Stars) wakati wanaume ni
Alpha Kisusi (Vijana) na Filbert Mwaipungu na Gilbert Batungi (ABC).
Mchezo wa netiboli wanawake ni Lilian Sylidion, Doritha Mbunda wakati gofu
kwa wanawake ni Madina Idd, Hawa Wanyeche na Ayne Magombe na
wanaume ni Frank Roman, Nuru Mollel na Issac Anania huku mchezo wa gofu
wa kulipwa wanaowania tuzo ni Fadhili Saidi Nkya, Yasini Salehe na Hassani
Kadio na Olimpiki maalum ni Ahmada Bakar, Amina Daud Simba na Othman
Ally Othman.
Paralimpiki kwa wanaume ni Zaharani Mwenemti, Joseph Nziku na Yohana
Mwila wakati wanawake ni Faudhia Chafumbwe, Siwema Kilyenyi na Janeth
Madise huku mchezo wa ngumi za ridhaa wamo Suleiman Kidunda, Victor
Njaiti na Abdalah Kassim na waogeleaji wanawake Magdalena Moshi, Gouri
Kotecha na Mariam Foum na wanaume ni Ammaar Ghadiyali na Omari
Abdalah.

No comments:

Post a Comment