KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 24, 2012

SIMBA YAMNASA KIBOKO YA YONDANI TOKA DRC

KLABU ya Simba imefanikiwa kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Masombo Lino kutoka Daring Club Motema Pembe.
Beki hilo la kati ambalo lilipiga soka ya uhakika mwaka jana wakati Simba ilipokutana na DC Motema Pembe katika mechi ya mchujo kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, lilitua jana Dar es Salaam na leo imeelezwa limesaini mkataba.

Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga amesema beki huyo alikuwa na mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa klabu yao, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ leo baada ya kutua jana na inawezekana amesaini mkataba wa miaka miwili.

“Masombo amekuja jana saa mbili usiku, alikuwa ana mzungumzo na Makamu Mwenyekiti, inawezekana leo akawa amesaini mkataba wa miaka miwili kama wameafikiana,”alisema Kamwaga.

Simba, mabingwa wa Ligi Kuu ya Bara, wanamsajili beki huyo kuziba pengo la beki wao hodari, Kelvin Patrick Yondan ambaye amehamia kwa wapinzani, Yanga.

Habari hii ni kwa mujibu wa mtandao wa www.binzubeiry.blogspot.com.

No comments:

Post a Comment