KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, June 22, 2012

Yondan aanza mazoezi Yanga

Beki mpya wa klabu ya Yanga, Kelvin Yondan ameanza rasmi mazoezi na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Kagame.
Yondan, ambaye gazeti moja la michezo liliripoti kwamba ametekwa na Simba, alianza mazoezi jana asubuhi kwenye uwanja wa Jangwani uliopo makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa mtandao wa www.binzubeiry.blogspo.com, mazoezi hayo halihudhuriwa na mamia ya mashabiki wa Yanga waliokuwa na hamu kubwa ya kumuona mchezaji huyo.
Yondan ni miongoni mwa wachezaji wawili wapya waliosajiliwa na Yanga kutoka katika klabu ya Simba, ambayo ni mahasimu wao wakubwa. Mwingine ni kipa Ally Mustafa 'Barthez', aliyeanza mazoezi tangu juzi.
Yanga inajiandaa kwa michuano ya Kombe la Kagame, inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Dar es Salaam. Timu zingine za Tanzania Bara zitakazoshiriki michuano hiyo ni mabingwa wa ligi kuu, Simba na washindi wa pili, Azam.

No comments:

Post a Comment