KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 11, 2012

FIFA YANOA WAAMUZI WAKE NA WATOTO WA TWALIPO

Waamuzi 54 wanashiriki kozi ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) iliyoanza leo (Juni 11 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kozi hiyo itakayomalizika Juni 14 mwaka huu inaendeshwa na wakufunzi
wawili kutoka FIFA wakisaidiwa na wakufunzi wengine wanne wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Wakufunzi wa FIFA ni Carlos Henriques na Mark Mizengo. Wakufunzi kutoka TFF ni Kapteni mstaafu Stanley Lugenge, Leslie Liunda, Soud Abdi na Riziki Majala.

Waamuzi wanaoshiriki ni 14 wa Tanzania wenye beji za FIFA ambao ni
Erasmo Jesse, Ferdinand Chacha, Hamis Changwalu, Hamis Maswa, Israel
Mujuni, John Kanyenye, Josephat Bulali, Judith Gamba, Mwanahija Makame,
Oden Mbaga, Ramadhan Ibada, Saada Tibabimale, Samuel Mpenzu na Sheha
Waziri.

Washiriki wengine ni 20 wa daraja la kwanza (class one), kati ya hao watano
wanatoka Zanzibar. Pia wamo waamuzi chipukizi (watoto) 20 ambao
mwaka jana walitumika katika michuano ya Kombe la Uhai na Copa
Coca-Cola.

No comments:

Post a Comment