KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 18, 2012

Wakazi wa arusha waipokea kwa shangwe huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5

.Mmoja wa wasanii anaeitikisa anga ya muziki wa hip hop nchini,anatamba na tuzo mbili za muziki huo huo huo wa hip hop,Roma akiamsha amsha hadhira kubwa ya watu iliojitokeza jioni ya leo kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel,Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika jana kwenye viwanja vya NMC mjini Arusha na kuhudhuriwa na umati mkubwa watu.

Sehemu ya Wakazi wa Arusha wakishangilia ujio wa huduma mpya ya Airtel Supa5



.Anajiita Mwamba wa Kaskazini,Msanii mwingine mahiri katika miondoko ya muziki wa hip hop nchini,Joe Makini akitumbuiza kwenye jukwaa jana kwenye viwanja vya NMC jijini Arusha,wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 kwa wakazi wa Arusha.


Wakazi wa jiji la Arusha wakiendelea kuhamia na kujiunga kwa wingi na Airtel.


Sehemu ya Wakazi wa Arusha wakishangilia ujio wa huduma mpya ya Airtel Supa5


Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume Halisi lenye maskani yake Temeke,jijini Dar es Salaam,Juma Nature akiwarusha baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya NMC, wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 kwa wakazi wa Arusha.


Pichani kati ni Meneja Mauzo wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Airtel-Arusha,Bwa Stephen Akyoo akiwa katika picha ya pamoja na washindi walioielezea vyema huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 na kujishindia zawadi ya simu aina Samsung.Kulia ni Lucas George na shoto ni Swalehe Mohamed.


Meneja Mauzo wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Airtel-Arusha,Bwa Bw Stephen Akyoo akimkabidhi simu aina ya Samsung mmoja wa wakazi wa Arusha aitwaye Lucas George mara baada ya kushinda shindano la kughani ,wakati kampuni ya simu za mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Jiunge na Supa5,uliofanyika kwenye viwanja vya NMC mjini Arusha. Huduma ya Airtel Jiunge na Supa5 ilizinduliwa rasmi hivi karibuni jijini Dar na baadaye kuendelea kuzinduliwa katika mikoa mbalimbali kwa ajili ya kuwapa kilicho bora wateja wake popote pale walipo.















No comments:

Post a Comment