KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, October 4, 2011

VAZI LA TAIFA

Kwa miaka mingi sasa, nimeshuhudia wabunifu wetu wa mavazi wakihangaika kubuni vazi letu la kitaifa, ambalo halitafanana na vazi la nchi zingine za kiafrika. Kumbe hatukuwa tukifahamu kwamba, Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alishatubunia vazi hili miaka mingi sana, tatizo ni kwamba tumeshindwa kutambua hilo. Nilikutana na picha hii hivi karibuni kwenye makumbusho ya Mwalimu Nyerere iliyopo nyumbani kwake Mwitongo katika kijiji cha Butiama kilichopo Musoma Vijijini mkoani Mara. Nikapata hamu ya kupiga picha pembeni ya picha hii. Kazi kwenu wale mnaohangaika kubuni vazi la Taifa. Mwalimu Nyerere alikuwa akiona mbali. Alishatubunia vazi letu. Hebu litazameni linavyopendeza.

No comments:

Post a Comment