KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 13, 2011

Nora amaliza bifu lake na P-Square


LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI na mwanamuziki machachari wa Nigeria, Steph Nora Okere amekiri kumaliza bifu kati yake na wanamuziki wa kundi la P-Square, Peter na Paul Okoye.
Meneja wa Nora, Ope Banwo alisema wiki hii mjini hapa kuwa, wameamua kutoendelea na mpango wa kuwafungulia kesi wanamuziki hao.
“Hakuna tena kesi. Suala hilo limemalizika. Wamefikia mwafaka. Wanaendelea na urafiki wao,” alisema msemaji huyo katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari.
Uamuzi huo wa Nora umekuja siku chache baada ya kuwepo na taarifa kwamba, Peter na Paul wameiba wimbo wa mwanadada huyo na kuurekodi kwenye albamu yao mpya.
Nora aliwaeleza waandishi wa habari hivi karibuni kuwa, aliupeleka wimbo huo, unaojulikana kwa jina la Jeje kwa Jude Okoye, kama mkubwa wa wanamuziki hao wawili ili ausikilize na kumpa ushauri.
Alisema alikuja kushangaa kusikia wimbo huo umo kwenye albamu mpya ya P-Square, inayokwenda kwa jina la The Invasio, ukiwa umeongezewa nakshi kidogo.
Nora alisema alipanga kuzindua albamu yake mpya Desemba mwaka huu, ikiwa na kibao hicho, ambacho Jude alimshauri akifanyie marekebisho, akakubali.
“P-Square ni kundi kubwa na maarufu, halipaswi kufanya hivyo kwa wasanii wanaochipukia na rafiki zao. Niliwaamini, lakini wamenifanyia kitendo cha kihuni,”alisema Nora.
Naye msemaji wa P-Square, Bayo Adefu amesema hawakuwa na tatizo na Nora na kwamba walishangaa kusoma taarifa za kuibiwa wimbo wake kwenye vyombo vya habari.
“Ukisikiliza nyimbo hizi mbili, utagundua kwamba hazifanani kabisa,”alisema Bayo.

No comments:

Post a Comment