KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, October 13, 2011

GURUMO KUPEWA TUZO KESHO



KAMPUNI ya Tanzania Distillers Limited (TDL) imeandaa bonanza maalumu kesho kwa ajili ya kumzawadia mwanamuziki mkongwe nchini, Muhidin Gurumo.
Mratibu wa tamasha hilo, Mohamed Pizzaro alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, tamasha hilo litafanyika kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni.
Kwa mujibu wa Pizzaro, tuzo hiyo itakabidhiwa kwa Gurumo na Mkurugenzi Mtendaji wa TDL, David Mgwasa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.
Gurumo, ambaye kwa sasa ni kiongozi wa bendi ya Msongo Ngoma, amewahi kuimbia bendi mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na Mlimani Park Orchestra na Orchestra Safari Sound (OSS).
Mkongwe huyo alianza kujihusisha na masuala ya muziki miaka ya 50, lakini bendi yake ya kwanza ilikuwa Kilimanjaro Chacha, aliyojiunga nayo mwaka 1961 kabla ya kujiunga na Kilwa Jazz mwaka 1963.
“Zawadi gani atakayokabidhiwa, hilo inajua kampuni ya TDL na Mgwasa mwenyewe, lakini ni ‘surprise’ kwa mashabiki na Gurumo mwenyewe,” alisema Pizzaro. Alisema shamrashamra za tamasha hilo, ambalo pia litakuwa la kumuenzi Baba wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere litapambwa na burudani ya muziki kutoka bendi ya Msondo Ngoma.
Mbali na burudani hiyo, alisema kutakuwepo na mechi ya kirafiki kati ya timu za maveterani za Kigamboni na Namanga na kati ya Brake Pointi na Mango Garden.

No comments:

Post a Comment