KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, June 14, 2012

Sijakuza matiti yangu-Ebube


LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu anayechipukia nchini Nigeria, Ebube Nwagbo amesema kamwe hajawahi kufanya operesheni ya kukuza matiti yake ili aonekane kuwa na mvuto.
Akihojiwa na mtandao wa naijerules hivi karibuni, Ebube alisema hivyo ndivyo ulivyo mwonekano wa kifua chake na hafikirii kufanya kitu kama hicho.
Ebube alisema swali kama hilo pia aliwahi kuulizwa na mama yake mzazi, siku alipoona picha yake gazetini, lakini alisisitiza kwamba jibu lake ni hapana.
Alisema inawezekana matiti yake yamekuwa yakionekana makubwa kutokana na aina ya nguo anazovaa.
“Hata mama yangu alinipigia simu na kuniuliza iwapo nilifanya operesheni ya kukuza matiti yangu,”alisema Ebube.
“Nafikiri ni kwa sababu ya aina ya nguo niliyovaa. Nilikuwa nimevaa bikini. Kwa sasa sivai tena nguo za aina hiyo,”aliongeza. Alipoulizwa kuhusu njia anazotumia katika kutunza urembo wake, Ebube alisema analala vizuri, kuwa na muda mrefu wa mapumziko na pia kula matunda kwa wingi.
“Sinywi maji mengi na ninakula chakula kizuri. Nakula vyakula vyenye kujenga afya,”alisema.
Ebube alisema japokuwa matarajio ya wanawake wengi ni kuolewa, kwake halipi uzito suala la kufunga ndoa. Alisema atafunga ndoa mara tu atakapokuwa tayari kufanya hivyo.
Mwanadada huyo alisema anaona fahari kuwa miongoni mwa waigizaji wa Nollywood na kuwapongeza wasanii wenzake waliopata mafanikio.

No comments:

Post a Comment