KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, June 24, 2012

Simba yaichapa Toto African 2-0

MABINGWA wa ligi kuu ya Tanzania Bara, Simba jana waliichapa Toto African ya Mwanza mabao 2-0 katika pambano kali la kirafiki lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza ya kirafiki kwa Simba katika ziara yake ya mikoa ya kanda ya ziwa iliyoanza jana (Juni 22) na kumalizika keshokutwa.
Wekundu wa Msimbazi walianza pambano hilo kwa kasi na iliwachukua dakika 17 tu kuandika bao la kwanza lililowekwa kimiani na Uhuru Selemani aliyemalizia vizuri pasi ya Abdallah Juma.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Simba ilikuwa inaongoza kwa bao hilo moja.
Katika kipindi cha pili, Simba ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Abdallah Seseme na Hassan Khatib na nafasi zao kuchukuliwa na William Lucian (Gallas) na Jonas Mkude.
Mabadiliko hayo yalizaa matunda kwani katika dakika ya 48, Simba iliandika bao la pili lililofungwa na Salim Kinje, mchezaji mpya wa Simba aliyesajiliwa kutoka AFC Leopards ya Kenya.Kinje alifunga bao hilo akiunganisha moja kwa moja kutoka nje ya 18 pasi ya kichwa kutoka kwa Uhuru.
Katika pambano hilo wachezaji waliosajiliwa msimu huu walikuwa ni Waziri Hamad, Paulo Ngalema, Kiggi Makassy, Kinje na Abdallah Juma.Wachezaji wawili wa kikosi cha vijana Simba maarufu kwa jina la U-20, Haruna Chanonga na Lucian pia walicheza mechi yao ya kwanza kwa kikosi cha wakubwa.
Juni 24 Simba itaingia kwenye uwanja wa Kambarage, Shinyanga kupambana na mabingwa wa soka wa Uganda, Express
Simba iliwakilishwa na ; Waziri, Hassan (Gallas), Ngalema (Omar Waziri), Obadia Mungusa, Haruna Shamte, Amri Kiemba (Edward Christopher), Chanonga, Seseme (Kiggi), Abdallah (Ramadhani Salum), Kinje na Uhuru.
Habari hizi ni kwa mujibu wa blogu ya www.binzubeiry.blogspot.com

No comments:

Post a Comment