Msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Dogo Janja amethibitisha rasmi kutengana na kundi la Tip Top Connections lenye maskani yake Manzese, Dar es Salaam baada ya kukorofishana na kiongozi wa kundi hilo, Madee.Dogo Janja alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, baada ya kutengana na Tip Top, aliamua kurejea nyumbani kwao Arusha kabla ya kurejeshwa tena Dar na promota mmoja maarufu wa muziki.
Alimtaja promota huyo kuwa ni mmiliki wa kundi la Watanashaji, Juma wa Musoma. Amemshukuru promota huyo kwa uamuzi wake huo, ambao amesema umelenga kuendelea kukuza kipaji chake.
No comments:
Post a Comment